SARE NA SIMBA YAMTIA MZUKA LWANDAMINA KUSAKA MASTRAIKA ZAIDI YANGA SC

KOCHA wa Yanga, George Lwandamina amesema timu yake ina kikosi imara ambacho wakati wowote kinaweza kuifunga Simba lakini kitendo cha kuwakosa wachezaji wake watatu ndiyo iliyowanyima ushindi na sasa amataka mchakato wa kusajili mastraika ufanyike kwa haraka.

Kocha huyo raia wa Zambia amesema endapo kikosi chake kingekuwa kamili kwa kuwepo Donald Ngoma na Amissi Tambwe hata kwa dakika 20, ilikuwa inatosha kuwamaliza Simba ambao amedai hawana la kutisha.

Lwandamina amesema kwa sasa anachotaka ni kuona viongozi wa klabu hiyo wanasaka mshambuliaji wa haraka ambaye atakuja kusaidiana na Chirwa na Ajib.

“Tulijipanga kuwafunga Simba na tulifanikiwa kuwashika katika maeneo yote lakini tulikuwa kama tumecheza pungufu nafurahi kuona Ajib na Chirwa wakifanya kazi kubwa,” alisema Lwandamina.


“Chirwa aliumia muda mrefu lakini hakukuwa na namna alihitajika lakini kama tungekuwa na huduma ya washambuliaji wengine ambao bado ni majeruhi hata kwa dakika chache tu tungefanya kitu tofauti.”

No comments