SIKIA HII... ETI TIN WHITE "HAPENDAGI" KUPIGA PICHA NA RICH MAVOKO JAPOKUWA NI NDUGU!

MCHEKESHAJI mahiri Tin White amefunguka na kusema kuwa hana utamaduni wa kupenda kupiga picha ya pamoja na Rich Mavoko ingawaje ni ndugu yake wa damu.

Rich mavoko na Tin ni watoto wa mama mmoja ambapo Tin ni wa pili kuzaliwa na huku Mavoko akiwa mtoto wa tano.

“Si kwa ubaya bali binafsi nimejiwekea hivyo tangu nikiwa mdogo kabisa ambapo kiukweli unaweza ukanambia nitafute picha niliyopiga nae pamoja hata kwa kuniahidi mamilioni ya pesa lakini nikaikosa,” amesema Tin.


Mbali ya Mavoko, vilevile Tin ni ndugu wa damu wa mkali wa filamu, mwanadada Ummy Wencelaus “Dokii” ambaye ni binamu yao, wote wakiwa ni wajukuu wa mzee Lusinga.

No comments