SIMBA SC, NJOMBE MJI ZATIA AIBU KUGOMBEA KUSHUSHA WACHEZAJI UWANJA WA UHURU

MAKOMANDOO wa Timu za Simba na Njombe Mji FC Jumamosi walitia fora kwenye uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam wakati walipotunishiana misuli huku kila upande ukitaka wachezaji wake wawe wa kwanza kuingia getini.

Askari walilazimika kufanya kazi ya ziada kuwazuia makomandoo hao ambapo kila upande ulitaka wachezaji wake waingie kwanza ndipo wengine wafuate.

Madereva wa gari zote mbili za Simba na Njombe walizikutanisha gari zao uso kwa uso wakigombea kuwa wa kwanza kushusha wachezaji waliokuwa ndani ya magari hayo.

Sababu ya kuwa wa kwanza kuingia uwanjani imetafsiriwa na mashabiki kuwa huenda ni masuala ya kiimani ya timu hizo mbili zilizokuwa zikikutana katika mchezo wa Ligi Kuu bara ambayo imefikia mzunguko wa saba.


Hata hivyo katika vuta nikuvute hiyo ya makomandoo, timu ya Simba ilifanikiwa kuwa ya kwanza kuingiza wachezaji wake kisha ikifuata Njombe na baadaye mlango ukafungwa.

No comments