SIMBA YAANZA "KUIMBWERA" MTIBWA SUGAR

KATIKA mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba inatarajia kukutana na timu ya Mtibwa Sugar, mchezo ambao umeanza kulipa wasiwasi benchi la ufundi la mtaa wa Msimbazi kuhofia kushuka kileleni.

Kocha msaidizi wa timu ya Simba Jackson Mayanja amesema kwamba mechi dhidi ya Mtibwa inaweza kuwa hatima yao ya kuendelea kukaa kileleni au la katika mzunguko huu wa kwanza wa Ligi.

Katika mechi iliyopita, Mtibwa ililazimisha sare ya bila kufungana walipocheza na mabingwa watetezi Yanga na katika mechi inayofuata watawavaa Simba.

“Ni mchezo mgumu lakini tumejidhatiti kuhakikisha tunachukua pointi zote tatu katika mchezo huo kwasababu tumeupa kipaumbele na kutufikisha na mechi zingine,” alisema kocha huyo.

“Mtibwa sio timu ya kubeza maana ikiwa tutapoteza mechi hiyo tutapoteza pia nafasi ya kukaa kileleni mwa Ligi,” aliongeza.


Simba ilikuwa Kanda za Ziwa ambapo imecheza mechi mbili na kuambulia alama 4 baada ya kupata sare kwa Mbao FC, kisha ushindi wa Stand United.

No comments