TAMBWE ATUMA SALAMU KAGERA SUGAR NA STAND UNITED

MSHAMBULIAJI wa Yanga Amiss Tambwe amewatumia salam Kagera Sugar na Stand United kuwa amerudi akiwa na hamu ya kuchana nyavyu na kwamba sasa mashabiki wa Yanga watulie kazi inaanza.

Tambwe amesema kwasasa amefanikiwa kupona kabisa na kwamba akili yake inawaza kufunga tu hakuna lingine.

Tambwe amesema anafurahi kurudi katika kikosi chake ambapo anawajua Ibrahimu Ajib na Obrey Chirwa kwamba makali ya safu yao yanarudi rasmi.

Raia huyo wa Burundi amesema alikuwa anaumizwa na kikosi chao kusaka nguvu yake na sasa mashabiki wa Yanga watulie na kuja kwa wingi kwamba wanajipanga kuanza dozi za maana.

No comments