Habari

TANZANIA BAND FESTIVAL BABA YA MATAMASHA YA DANSI KUANZA KURINDIMA KAHAMA IJUMAA HII … Jumamosi Mwanza, Jpili Dodoma

on

Lile tamasha la muziki wa dansi lililopewa jina la Tanzania Band
Festival ambalo linafanyika kwa mwaka wa pili sasa tangu lianzishwe mwaka jana,
linaanza kutimua vumbi Ijumaa hii.
Kwa mara ya kwanza, Tanzania Band Festival ilifanyika mwezi Julai
mwaka jana ndani ya viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam huku zaidi ya
bendi 10 zikishiriki.
Lakini safari hii, tamasha hilo linajitanua zaidi ambapo sasa
litafanyika katika mikoa kadhaa tofauti na mwaka jana.
Tanzania Band Festival itaanza kurindima mjini Kahama Ijumaa hii
Oktoba 6 katika Uwanja wa Kahama na kufuatiwa na show ya jijini Mwanza Oktoba 7
ndani ya Rock City Mall.
Bendi zitakazoshiriki maonyesho ya Mwanza na Kahama ni FM Academia,
Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Malaika Music Band na B Band.
Saluti5 imefahamishwa kuwa baada ya maonyesho ya Kahama na Mwanza,
bendi hizo zitalekea Dodoma ambapo Tanzania Festival Band itafanyika Jumapili
ndani ya Kisasa Cape Town Complex kabla ya kuelekea mikoa mingine
itakayotangazwa hapo baadae.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *