TANZANIA BAND FESTIVAL KUITEKA MWANZA LEO USIKU


Baada ya jana kurindima kwenye mji wa Kahama, lile tamasha la muziki wa dansi lililopewa jina la Tanzania Band Festival, leo usiku litanguruma jijini Mwanza.

Tanzania Band Festival jana ilikonga nyoyo za mashabiki wa Kahama katika  Uwanja wa Taifa Kahama, lakini mpango mzima ni Mwanza leo ndani ya Rock City Mall.

Bendi zitakazoshiriki zitakazoumana Mwanza ni Kahama ni FM Academia, Twanga Pepeta, Msondo Ngoma, Malaika Music Band na B Band.

Saluti5 imefahamishwa kuwa baada ya maonyesho ya Kahama na Mwanza, bendi hizo zitalekea Dodoma ambapo Tanzania Festival Band itafanyika kesho usiku ndani ya Kisasa Cape Town Complex.

No comments