TFF YAIKATA MAINI YANGA MECHI DHIDI YA SIMBA

JITIHADA za klabu ya Yanga kutaka mechi yake dhidi ya Simba SC ichezwe kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza zimeonekana kugonga mwamba baada ya Shirikisho la soka nchini kusisitiza kwamba mechi hiyo itachezwa kwenye uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.

Yanga ambao ndiyo wenyeji wa mechi hiyo itakayopigwa Oktoba 28, mwaka huu walikuwa wameomba kwa TFF kwamba mechi yao ichezwe kwenye uwanja huo, lakini TFF wamekataa ombi hilo kwasababu halina mashiko.

Imedaiwa kwamba Yanga wameshaanza kushtuka kwamba hawana uwakika wa kushinda kwenye uwanja wa uhuru na hivyo walikuwa wanajaribu kusaka namna ya kuondoka katika jiji la Dar es Salaam ambako wanadhani kwamba wanaweza kushinda.


Lakini baadhi ya wanachama wa samba hata kama mechi hiyo itachezwa nje ya Tanzania lazima Yanga wafungwe kutokana na Simba kuwa na kikosi imara zaidi.

No comments