THIERRY HENRY ASEMA ANTHONY MARTIAL NI BORA KULIKO YEYE KATIKA UMRI WA MIAKA 21


THIERRY HENRY amesema katika umri wa miaka 21 alionao Anthony Martial, ni mchezaji bora zaidi kuliko yeye alivyokuwa kwenye umri huo.
Henry amekuwa akifuatilia maendeleo ya  Martial tangu alipotua Manchester United kwa pauni milioni 50 miaka miwili iliyopita.
"Anthony Martial ni bora kwa mbali sana kuliko mimi wakati nilipokuwa na umri wa miaka 21, anaweza kuwa mchezaji bora duniani," anaeleza Henry.

No comments