Habari

TONI KROOS ASEMA ALIKUWA SAHIHI KUIKIMBIA BAYERN MUNICH NA KUITOSA MANCHESTER UNITED

on

TONI KROOS  anaamini alikuwa sahihi kuihama Bayern Munich na pia hakukosea kuichagua Real Madrid badala ya Manchester United.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliondoka Bayern Munich mwaka 2014 na kutua Real Madrid kwa dau la pauni milioni 20 na kuiacha kwenye mataa Manchester United ambayo ilimsumbukia kwa dirisha zima  la usajili wa majira ya kiangazi mwaka huo wa 2014.
Kroos anasema: “Kuondoka kwangu Bayern kulikuwa ni sahihi na nilichagua timu sahihi, hakuna shaka juu ya hilo, tazama mataji niliyotwaa na Real Madrid.
“Ni wazi kuwa unapoamua kwenda nje ya nchi na kujiunga na klabu kubwa, inamaanisha kuwa umepiga hatua katika soka lako.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *