TOTTENHAM YAIBANA REAL MADRID NYUMBANI … APOEL Nicosia 1 - 1 Borussia Dortmund


Real Madrid ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, ililazimika kukubali sare ya 1-1 dhidi ya Tottenham katika mchezo wa kundi H wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Tottenham ilitangulia kwa goli la zawadi kunako dakika ya 28 baada ya beki Raphael Varane kujifunga, lakini Cristiano Ronaldo akaisawazishia Real Madrid kwa mkwaju wa penalti dakika ya 43.

Katika mchezo mwingine wa kundi H, timu za APOEL Nicosia na Borussia Dortmund nazo zilitoka sare ya 1-1.

No comments