TWANGA PEPETA YAPATA CHIMBO JIPYA LA JUMAMOSI, YAONDOKA MANGO GARDEN


Bendi ya The African Stars “Twanga Pepeta” imeuhama ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni na sasa itakuwa ikipatikana Kijitonyama kila siku za Jumamosi.

Meneja wa Twanga Pepeta Martin Sospeter ameiambia Saluti5 kuwa sasa ukumbi wao wa kila Jumamosi ni Vision Plus Lounge ambao zamani ulijulikana kama Miti Mirefu.

Martin amesema Jumamosi hii watakuwa mjini Tanga lakini kuanzia Jumamosi ya Oktoba 21 watakuwa wakipatikana Vision Plus Lounge.


No comments