USIKU WA NYUMBANI NI NYUMBANI KUITIKISA CLUB MASAI JUMATANO HII …Chokoraa na bendi yake dhidi ya Wakali Wao


Hatimaye lile onyesho la “Usiku wa Nyumbani ni Nyumbani” limewadia ambapo Khalid Chokoraa atavamia Meridian Hotel (Club Masai), Kinondoni Jumatano hii Oktoba 4.

Kama ilivyolezwa hapo awali kuwa kwa muda mrefu Chokoraa amekuwa ni mtoto wa nyumbani hapo Meridian Hotel tangu akiwa na bendi ya Mapacha Watatu na baadae Twanga Pepeta kabla hajaamua kuanzisha bendi yake binafsi Mapacha Watatu Original.

Chokoraa anarejea nyumbani akiwa na bendi yake katika show ya pamoja na Wakali Wao Modern Taarab chini yake Thabit Abdul.

Je nani atafunika zaidi? Mapacha Watatu ya Chokoraa au Wakali Wao ya Thabit Abdul? Jibu ni Jumatano usiku ndani ya Meridian Hotel (Club Masai), Kinondoni.

No comments