VICTORIA SOUND YAANIKA RATIBA YAO WIKIENDI HII


VICTORIA Sound Band imeanika ratiba zake za maonyesho kwa wiki hii ambapo leo Ijumaa wanatarajiwa kuwasha moto mkali wa burudani ndani ya kiwanja cha kujidai cha Scorpion Pub, Mbagala Charambe, Mbagala, jijini Dar es Salaam.

“Jumamosi tutarindima ndani ya Masebuka Bar maweneo ya Mbagala Kizuiani na Jumapili tutamalizia uhondo wetu wa wiokiendi katika ukumbi wa Kiburugwa Inn, Mbagala Kiburugwa,” amesema Jonas Mnembuka, kiongozi mwandamizi wa Victoria Sound.


Kiongozi huyo amesema kuwa, katika shoo zote hizo, bendi yake hiyo inayotumia mtindo wa “Wazee wa Murua” itarindimisha muziki katika mtindo wa bandika bandua yaani bila kupumzika kuanzia mwanzo hadi mwisho, huku kiingilio kikiwa ni bure.

No comments