VICTORIA BECKHAM AKIRI UGUMU WA KUISHI BILA KITOTO CHAKE

MWANAMITINDO Victoria Beckham, mke wa David Beckham amesema kuwa anapata wakati mgumu kuishi bila mwanae wa kiume, Brooklyn ambaye yupo masomoni nchini Marekani.

Staa huyo wa kundi la zamani la “Spice Girls” amekuwa akitumia muda mwingi kushea picha na mwanae kwenye mitandao ya kijamii.

Brooklyn mwenye miaka 18, ameiacha familia nchini Uingereza na yeye yupo Marekani katika jiji la New York kwa ajili ya masomo ya chuo akisomea fani ya sanaa.


“Nimeshazoea kuwa na Brooklyn, nimekuwa nikifanya mambo mengi sambamba na yeye, inanipa shida kuwa nae mbali,” alisema Victoria.

No comments