VIDEO: MSAFIRI DIOUF: REMIX YA NYIMBO ZANGU WATAFANYA WANANGU …asema yeye hajakaukiwa nyimbo mpya


Msanii wa zamani wa Twanga Pepeta, Msafiri Diouf amesema ana utajiri mkubwa wa tungo na hivyo hana mpango wa kurudia (remix) ya nyimbo zake za zamani.

Akiongea katika ofisi za Saluti5, Diouf akasema katika muziki alionao moyoni mwake, basi hizi alizotoa na Twanga Pepeta ni asilimia 30 za muziki wake.

“Bado nina asilimia 70, nina nyimbo nyingi sana ambazo zinanitekenya kwenye mwili wangu, kwahiyo siwezi kurudia nyimbo,” alisema Diouf ambaye kwasasa anafanya muziki nchini Uingereza.

“Zile nyimbo nilizotoa na Twanga Pepeta watakuja kuzirudia wanangu. Kama bado zitakuwa na ubora hadi muda huo basi kina Vanessa na wangu wengine ndiyo watazirudia kama alivyofanya Papy Kocha kurudia nyimbo za baba yake,” aliongeza Diouf ambaye yupo nchini kwa mapumziko ya miezi mitatu.No comments