PICHA 11: TWANGA PEPETA WALIVYOFUNGA PAZIA LA TZ BAND FESTIVAL NDANI YA DODOMA


The African Stars “Twanga Pepeta” ndiyo waliopewa jukumu la kuhitimisha show ya Tanzania Band Festival mjini Dodoma ndani ya Kisasa Capetown Complex.

Twanga wakavutia sana kwa namna walivyojua kuchagua nyimbo pendwa zinazofahamika na mashabiki wengi.

Walianza na “Safari” na kufuatiwa na “Walimwengu” ikawa ni faida nzuri kwao kwa namna mashabiki walivyokuwa wakishangilia. Baadae wakamalizia na “Password”.

Uwepo wa Msafiri Diouf nao ukaongeza chachu ya kuwakuna vilivyo mashabiki ambapo kwao wao hiyo ilikuwa ni kama sapraiz fulani.
 Luizer na Chocky
 Jojoo Jumanne kwenye bass, Kirikuu kwenye tumba
 Kalala Jr akitupia masauti yake
 Chocky na Diouf wakipagawisha
 Diouf akishambulia jukwaa
 Kibosho kwenye drum
 Luizer Mbutu
 Twanga hawanaga mchezo kwenye kushambulia jukwaa
 Shakashia kwenye mpini wa solo
 Victor Nkambi kwenye kinanda
Hajj BSS akiimbisha mashabiki
No comments