Habari

WAMILIKI WA ARSENAL ‘WATUNISHIANA MISULI’ …hakuna mwenye mpango kuuza hisa

on

Mwekezaji wa pili
kwa ukubwa katika klabu ya Arsenal, Alisher Usmanov, anasema kuwa hajafanya
mazungumzo yoyote na mwenye hisa mkuu wa klabu hiyo Stan Kroenke kuhusu kumuuzia
kiwango chake cha hisa katika klabu hiyo.
Imeripotiwa kuwa
Kroenke ambaye anamiliki asilimia 67 za hisa aliwasilisha ombi la kutaka
kununua hisa za Usmanov ambazo ni asilimia 30.
Hatahivyo Usmanov
mwenye umri wa miaka 64 amesema kuwa maslahi yake katika Arsenal ni ya muda
mrefu.
”Nadhani umiliki
wangu wa asilimia 30 ni kitengo muhimu katika kulinda maslahi ya mashabiki
katika klabu hiyo”, alisema.
Licha ya kumiliki
hisa katika klabu hiyo Usmanov hayupo katika bodi ya klabu hiyo ambayo hufanya
maamuzi na amekuwa akimlaumu Kroenke kwa matokeo mabaya ya Arsenal uwanjani.
Raia huyo wa
Uzebek aliwasilisha ombi la pauni bilioni moja mnamo mwezi kuinunua klabu hiyo
lakini likakataliwa na Kroenke.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *