Habari

WANACHAMA YANGA KUCHANGIA MFUKO WA MAENDELEO YA KLABU YAO

on

WANACHAMA wa timu ya Yanga
wakiwakilishwa na mwenyekiti na katibu wa matawi kutoka jijini Dar es salaam
wameafikiana kuchangia klabu yao ili kutunisha mfuko wa kuiletea maendeleo klabu
yao.
Katika kikao kilichokaliwa Jumamosi makao makuu ya klabu mtaa wa Twiga na Jangwani kikiongozwa na
Makamu mwenyekiti, Clement Sanga, wanachama hao waliafikiana kutoa fedha kwa
ajili ya kukarabati uwanja wa Kaunda ili utumike kwa mazoezi ya wachezaji wake.
Wanachama hao wana hitaji
kikosi cha Yanga kifanye mazoezi kwenye uwanja wake wa Kaenda ili kuepuka
gharama kubwa ya kukodi kiwanja.
Moja kati ya mambo
waliyokubaliana ni kwenda kuhamasisha wanachama wenzao kuchangia upatikanaji wa
kifusi ili zoezi la ukarabati wa pichi ya mazoezi uanze haraka iwezekanavyo na
hadi kufikia msimu ujao kiwe kimekamilika.
Lakini wanachama hao
waliokuwepo kwenye mkutano walipeleka ujumbe wa kuonyesha wapo pamoja na
uongozi katika kupigania timu yao na uongozi katika kupigania timu yao
inayotetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na misukosuko mingi ya
kiuchumi waliyokumbana nayo.

Yanga inatarajia kucheza na
Kagera Sugar mchezo ujao wa Ligi Kuu bara ambapo mpaka hivi sasa wamecheza
jumla ya mechi 5 huku wakishinda mbili na kupata sare katika michezo yake
mitatu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *