WENGER ASHEREHEKEA MIAKA 21 ARSENAL KWA USHINDI DHIDI YA BRIGHTON


Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesherehekea miaka 21 ya kuiongoza Arsenal kwa ushindi wa 2-0 dhdi ya Brighton katika mchezo wa Premier League uliochezwa Emirates.

Baada ya piga nikupige langoni mwa Brighton ndani ya dakika ya 16, Nacho Monreal akafanikiwa kuifungia  Arsenal bao la kwanza baada ya walinzi wa Brighton kushindwa kuondoa mpira eneo hatari.

Alikuwa ni Alex Iwobi aliyeihakikishia ushindi Arsenal baada ya kufunga bao la pili muda mfupi baada ya mapumziko.

No comments