WILL SMITH NA FAMILIA YAKE WAPIGA MNADA VIWALO VYAO

RAPA na mcheza filamu za mapigano, Will Smith akiwa sambamba na familia yake wameanza zoezi la kupiga mnada nguo zao ili kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu.

Will Smith na Jada Pinket wameamua kupiga mnada nguo hizo na fedha kuziingiza kwenye mifuko ya kusaidia watu wanaoishi kwenye mazingira magumu nchini Marekani.


“Sisi kama familia tunaungana moja kwa moja na watu wanaoishi kwenye mazingira magumu,” ilisomeka sehemu ya taarifa fupi iliyotumwa na mastaa hao.

No comments