YAH TMK YAWAPELEKA CHANIKA PRINCE AMIGO NA KHADIJ YUSSUF


Wakali wa muziki wa mwambao, Yah TMK Modern Taarab, Ijumaa ya Oktoba 13 watafanya onyesho maalum kwa wakazi wa Chanika.

Meneja wa TMK Modern Taarab, Said Kessy Mnyama, ameiambia Saluti5 kuwa onyesho hilo litafanyika ndani ya ukumbi wa Butiama.

Said Kessy akadai katika onyesho hilo watakuwa na wasanii wawili waalikwa – Khadija Yussuf na Prince Amigo.


No comments