YANGA KEKO FURNITURE WACHOCHEA AJIB KUIBAMIZA SIMBA SC LEO

KUFUATIA uwezo ulioonyeshwa na mshambuliaji wa timu ya Yanga, Ibrahimu Ajib katika mechi za Ligi Kuu bara, wanachama wa klabu hiyo tawi la Keko Furniture wamesema kuwa watamuunga mkono staa huyo kuhakikisha anaifunga Simba kwenye mchezo wa leo.

Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa Ajib kukumbana na timu yake hiyo ya zamani baada ya ule wa Ngao wa Hisani uliomalizika kwa mikwaju ya penati.

“Raha yetu ni kuona moto alioanza nao Ajib unaendelea mpaka kwenye timu yake ya zamani ya Simba, tunataka afunge mechi ijayo ili tukae juu yao,” amesema mwanachama wa tawi hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Iddy.

“Tutashangilia kwa nguvu kila atakapogusa mpira, kwasababu hawa Simba wameongea sana wakati Ligi inaanza na kwa beki yao ile sidhani kama kuna mtu wa kumzuia Ajib,” aliongeza shabiki huyo.


Yanga na Simba zinakutana kwa mara ya kwanza katika michuano ya Ligi mwaka huu huku zote zkiwa na alama 15 kama ilivyo Mtibwa Sugar ya Morogoro.

No comments