YANGA YAIPONZA KAGERA SUGAR NA KUIFANYA IZIDI KUDIDIMIA

KATIKA msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, timu ya Kagera Sugar inashika mkia na hasa baada ya kufungwa na Yanga kwenye mchezo wa juzi uliochezwa kaitaba umesababisha waendelee kudidimia.

Msimamo wa Ligi sambamba na mechi ya Yanga juzi vinasababisha timu zingine kama Mbao zisimulikwe sana na mashabiki. Mjadala umekuwa Kagera Sugar peke yake.

Lakini takwimu zinaonyesha kuwa kikosi cha timu ya Mbao FC kutoka jijini Mwanza kimecheza mechi tatu mfululizo bila ushindi kwenye uwanja wake wa nyumbani, CCM Kirumba.

Mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya Mbeya City ambapo walilazimisha sare ya mabao 2-2.

Tangu wapate sare ya 2-2 wameendelea kupata sare katika mechi zote walizocheza CCM Kirumba.

 Walicheza na Prison wakapata sare kisha wakaja tena kucheza na Mbeya City wakaendelea kuambulia sare tu.


Kwa ujumla wake ni kwamba katika mechi sita za Ligi Kuu Mbao wameshinda mchezo mmoja tu dhidi ya timu dhaifu ya Kagera Sugar kisha wakafungwa mbili ugenini dhidi ya timu ya Singida United na Mtibwa Sugar.

No comments