ZLATAN IBRAHIMOVIC ANAKARIBIA KUREJEA UWANJANIZlatan Ibrahimovic amesherehekea miaka 36 za kuzaliwa kwake huku akiwathibitishia mashabiki wa Manchester United kuwa anakaribia sana kurejea uwanjani.

Mshambuliaji huyo aliyeumia goti msimu uliopita baada ya kuifungia United magoli 28 katika mechi 46, ametumia mitandao ya kijamii kuonyesha jinsi gani mguu wake ulioumia, uko imara.

Hata hivyo Ibrahimovic hata rejea uwanjani hadi jopo la madaktari wa United lijiridhishe kuwa nyota huyo amepona kabisa.

Ibrahimovic pia atakuwa na changamoto ya kupigania namba kufuatia namna safu ya ushambuliaji ya United ilivyoimarika.


No comments