4 STARS BAND YA NASSOR DIMOSO YANG’ANG’ANIWA MWANZA

MIEZI sita ya mkataba ulioingiwa kati ya bendi ya 4 Stars kutoka jijini Dar es Salaam na hoteli ya Buzuruga Plaza ya Mwanza unaonekana kuwa mdogo mno na huenda ukaongezwa, kufuatia mashabiki wa dansi “kuielewa” vilivyo bendi hiyo.

4 Stars Band iliyo chini ya mpapasa kinanda mahiri, nassor Dimoso imebakiza miezi miwili tu kumaliza mkataba huo na tayari uongozi wa hoteli ya Buzuruga umeonyesha nia ya kutaka kuketi tena mezani na 4 Stars Band kuzungumzia uwezekano wa kurefusha mkataba huo.

Dimoso ameiambia Saluti 5 muda mfupi uliopita kwa njia ya simu kuwa, baada ya wapenzi wa burudani kuonekana kuikubali bendi yao kwa kujitokeza kwa wingi wanapopiga, Buzuruga Plaza wameahidi kuwapa mkataba mwingine wa mwaka mmoja na zaidi utakaoambatana na ongezeko la maslahi.

“Tuko tunausikilizia uongozi wa hoteli na kama mambo yatakwenda poa huenda tukasalia hapa tena kwa mwaka mmoja ujao kwani inawezekana tukaongezewa kandarasi,” amesema Dimoso.

No comments