ABRAMOVICH AANZA KUMTESA KISAIKOLOJIA ANTONIO CONTE KUPITIA MGONGO WA MOURINHO


Jose Mourinho amealikwa mlo wa jioni na mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich baada ya mchezo wa leo jioni kati ya Chelsea na Manchester United utakaochezwa Stamford Bridge.
Hata hivyo haijajulikana kama Jose Mourinho amekubali mwaliko huo au la.
Mwaliko huo unakuja wakati ambapo kocha wa Chelsea Antonio Conte yupo kwenye shinikizo kubwa la kulinda kibarua chake.
Abramovich mara mbili amewahi kumwajiri na kumfukuza Mourinho, mara ya mwisho ilikuwa Disemba, 2015.
Bado Mourinho anabakia kuwa kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Chelsea - akitwaa taji la Premier League mara tatu, mataji matatu ya Ligi na FA katika vipindi vyake viwili alivyoifundisha timu hiyo.
Makazi ya familia yake yameendelea kubakia London wakati yeye akiishi katika hotel ya Lowry jijini Manchester.

No comments