AGUERO ASEMA: "NAWEZA KUSEPA MAN CITY NIKAREJEA NYUMBANI ARGENTINA MWAKA 2019"

STAA wa Manchester City, Sergio Aguero mwenye miaka 29, amesema kwamba anaweza kuondoka kwenye klabu hiyo mwaka 2019 na kurejea nchini kwao Argentina.

Mshambuliaji huyo anawaza kwenda kumalizia maisha yake ya soka katika klabu yake ya utotoni ya Independent iliyopo kwenye jiji la Buenos Aires.


Pamoja na jitihada zake za kufunga mabao muhimu lakini amekuwa hapewi sana kipaumbele na kocha Pep Guardiola kwenye kikosi chake cha kwanza.

No comments