ALEXIS SANCHEZ WA KAZI GANI TENA MANCHESTER CITY????


Wachambuzi wa soka wa England wanasema itakuwa ni maamuzi yasiyo na tija kwa kocha Pep Guardiola kumsajili Alexis Sanches dirisha la usajili la Januari.

Manchester City inaongoza Ligi Kuu ya England kwa pointi tano, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa ni kali kuliko timu yoyote ile England.

Kwa  mtaji huo, wachambuzi wa soka wanaamini Guardiola hahitaji kuvunja benki ili kuimarisha safu yake ya ushambuliaji.

Manchester City inakutana na Arsenal wikiendi huu huku gumzo kubwa likuwa ni mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanches ambaye amekuwa akiwaniwa na Guardiola.


City inatambia washambuliaji wake Kevin De Bruyne, David Silva, Raheem Sterling, Leroy Sane, Sergio Aguero na Gabriel Jesus ambao wameiwezesha timu hiyo kujikusanyia magoli 35 katika Premier Legue msimu huu. 

Guardiola amekuwa akimwinda Sanchez kwa udi na uvumba na iwapo atakuwa mvumilivu hadi mwishoni mwa msimu, basi huenda akamnasa bure mchezaji huyo kwa vile atakuwa amehitimisha mkataba wake wa Arsenal.


No comments