ALI KIBA ATESA TUZO ZA AFRIMA 2017 …amgaragaza Diamond Platnumz


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Ali Kiba ametwaa tuzo mbili za AFRIMA 2017 kati ya tatu alizoshindania.

Kiba alichaguliwa kuwania vipengele vya Best ‘African Collaboration’, ‘Best Artiste/Group in African RnB & Soul’ pamoja na ile ya ‘Best Artiste in African Contemporary’.

Katika tuzo hizo zilizofanyika Lagos, Nigeria usiku wa Jumapili, Kiba ambaye hakuwepo ukumbini, akanyakua tuzo za ‘Best African Collaboration’ kupitia wimbo wake wa “Aje” pamoja na ‘Best Artiste/Group in African RnB & Soul’ ambayo ndani yake mmoja wa washindani wake katika kipengele hiki alikuwa ni Diamond Platnumz wa Tanzania.

Mwimbaiji wa kike wa Tanzania Nandy akaibuka na tuzo ya 'The Best Female in Eastern Africa'.

Ukiondoa Kiba na Nandy, wasanii wengine wa Tanzania walioshiriki tuzo hizo wakiwemo Diamond, Msafiri Zawose, Darasa, Feza Kessy na Lady Jady, walitoka mikono mitupu bila kushinda hata tuzo moja.
Kipengele cha 'Best African Collaboration' alichoshinda Kiba
Kiba pia ameshinda kipengele cha ‘Best Artiste/Group in African RnB & Soul’ ambacho kilikuwa pia kilikuwa kikiwaniwa na Diamond Platnumz


No comments