ALICIA KEYS AKOMAA NA ZIARA ZA KUSAIDIA WATOTO WA MAZINGIRA MAGUMU

STAA anayetajwa kuwa na mvuto wa mapenzi Alicia Keys ameendelea na ziara zake ili kutunisha mfuko wa kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Hivi karibuni aliwatembelea watoto wagonjwa na kuimba nao pamoja wakiwa sambamba na wazazi wao huko San Francisco.

Alicia Keys baada ya kuimba na kundi hilo dogo alipiga picha ya pamoja kama sehemu ya ukumbusho kwa watoto hao wagonjwa.

Veronica Coreman na mtoto wake Tucker walikuwa sehemu ya watu waliokuwepo wakati Keys anatoa burudani.

Tucker anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ambao mpaka sasa ametimiza mwaka mzima bila kupona.


Keys na Lenny Kravitz wanafanya tamasha linaloitwa “The Concert for Kids” ili kutunisha mfuko wa kusaidia watoto.

No comments