ANTOINE GRIEZMANN SASA ANUKIA BARCELONA ...Manchester United imekula kwao
Antoine Griezmann anaonekana yuko mbioni kutua Barcelona dirisha la kiangazi baada ya klabu hiyo ya Catalan kupiga hatua nzuri ya mazungumzo na Atletico Madrid.

Mfaransa huyo anayewaniwa na Manchester United, moyo wake unaitaka safari ya kuondoka Atletico baada ya uhamisho wake kwenda Old Trafford kiangazi kilichopita kushindikana.

Kwa mujibu wa gazeti la Mundo Deportivo la Hispania, Barcelona sasa ipo kwenye nafasi nzuri ya kumsajili mshambuliaji huyo na kwamba kimsingi makubaliano ya awali yameshaafikiwa.No comments