ARSENAL, CHELSEA ZAINGIA VITANI KUSAKA SAINI YA KIPA PETER GULACSI WA RB LEIPZIG


ARSENAL na Chelsea ziko katika mbio kumfukuzia kipa wa klabu ya RB Leipzig, Peter Gulacsi na wawakilishi wao walikuwapo uwanjani Jumamosi wakati timu hiyo ya Ujerumani ikipoteza mechi mbele ya Bayern Munich.

The Gunners ipo katika harakati za kutafuta mbadala wa Petr Cech wakati Chelsea ikiwa katika tahadhari kwa kuwa kipa wake Thibaut Courtois hajasaini mkataba mpya na kuna tetesi za kufukuziwa na Real Madrid.

No comments