ARSENAL YAANZA KUGAWA DOZI KUBWA …YAIFUMUA HUDDERSFIELD 5-0


Mziki wa Arsenal sasa si wa kitoto na ni wazi kuwa Manchester United watakuwa na kibarua kizito Jumamosi pale watakapokabiliana na vijana hao wa Arsene Wenger.

Baada ya Arsenal kuichapa Tottenham wikiendi iliyopita, dozi ikahamishiwa kwa Huddersfield Town.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu uliochezwa Alhamisi usiku, Arsenal ikaichapa Huddersfield Town 5-0 ambapo mshambuliaji Olivier Giroud alifunga mara mbili.

Magoli mengine ya Arsenal yalifungwa na Alexandre Lacazette, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

No comments