ARSENAL YAFUKUZA MWIZI KIMYA KIMYA PREMIER LEAGUE …ALEXIS SANCHEZ AIBEBA TIMU


Arsenal ambayo msimu huu ilionekana kama si lolote si chochote, inazidi kukwea vidato kimya kimya kwenye msimamo wa Premier League ambapo sasa ipo nafasi ya nne.

Klabu hiyo ya London imeichapa Burnley 1-0 kwenye mchezo uliochezwa katika dimba la Turf Moor na sasa imebakiza pointi moja tu kuifikia Chelsea inayoshika nafasi ya tatu.

Alexis Sanchez ndiye aliyekuwa shujaa wa Arsenal baada ya kuifungia bao pekee kunako dakika ya 92 kwa mkwaju wa penalti.

No comments