ARSENAL YAICHINJA TOTTENHAM ...Alexis Sanchez, Mesut Ozil waamua kufanya kweli


Huku wachezaji waoonekana  wasaliti Alexis Sanchez na Mesut Ozil wakionyesha kiwango cha hali ya juu, Arsenal ikaitandika Tottenham 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Ikicheza kwenye uwanja wake wa nyumbani - Emirates Stadium - Arsenal ikapata bao la kwanza kunako dakika ya 37 kupitia kwa beki wake Shkodran Mustafi.

Ilipotimu dakika ya 41 Arsenal ikahitimisha kazi kwa kufunga bao la pili lililofungwa na Alexis Sanchez.

Kwa ujumla Tottenham ilizidiwa katika kila idara na kama Arsenal wangekuwa makini wangeweza kuibuka na ushindi mkubwa.

Arsenal (3-4-2-1): Cech; Koscielny, Mustafi, Monreal; Bellerin, Ramsey, Xhaka, Kolasinac; Ozil (Iwobi 84), A. Sanchez; Lacazette (Coquelin 73)

Tottenham (3-4-2-1): Lloris; D. Sanchez, Dier, Vertonghen; Trippier, Sissoko, Dembele (Winks 62), Davies; Eriksen, Dele 

No comments