ATHUMAN KAMBI WA MSONDO NGOMA AWAKUMBUKA "WALIOMTOA" KIMUZIKI

MWIMBAJI hodari wa Msondo Ngoma Music Band, Athuman Kambi amewakumbuka waliomsapoti kimuziki tangu wakati anaanza kujitumbukiza katika fani hiyo na kusema kuwa, anafanya jitihada kuhakikisha anauenzi mchango wao kwake.

Kwa hivi sasa, Kambi ambaye ni mahiri kwa uimbaji wa sauti za juu, ni kati ya waimbaji wanaovuta mashabiki wengi ndani ya Msondo Ngoma, hasa kutokana na uwezo wake mkubwa wa kuimba na kughani kiasi cha kujikuta anateka hisia za wengi.

“Nimetoka mbali sana kimuziki na kuna watu ambao, ingawa siwezi kuwataja mmoja mmoja kwa majina kutokana na wingi wao, lakini acha niseme kuwa nawashukuru sana,” amesema Kambi.


“Deni langu kwao ni kuhakikisha napiga mzigo kisawasawa kwa kuimba na kutunga nyimbo kali zitakazowafariji na kuonyesha kuwa mchango wao kwangu ulikuwa na maana kubwa,” ameongeza mwimbaji huyo anayetamba hivi sasa na kibao “Heshima Iko Wapi”.

No comments