AUDIO: KAPOSHOO AUNGURUMA CITY FM NA KUTAKA VITUO VYA RADIO VISIUKANDAMIZE MUZIKI WA DANSI …awachana wadau wa mitandaoni


Ijumaa jioni mpiga tumba wa FM Academia, Kaposhoo Tumba, alifanya mahojiano na kituo cha radio cha City FM cha jijini Dar es Salaam na kuzungumza mambo mengi ikiwemo suala la vituo vya radio kuukandamiza muziki wa dansi.

Akizungumza na watangazaji Irene Gabriel na Agape Msumari wanaoendesha kipindi bora cha muziki wa kiafrika – Tamba Afrika, Kaposhoo akasema kuna upungufu mkubwa wa muda wa kupiga muziki wa dansi kwenye vituo vya radio.

Aidha, Kaposhoo pia aliwachana mashabiki wanaowekeza nguvu kubwa mitandaoni hasa kwenye magroup ya facebook na whatsapp badala ya kuonyesha udau wao kwa kutembelea maonyesho ya bendi za dansi.

Msikilize hapo chini Kaposhoo anavyofunguka.

Kaposhoo (kushoto) akiwa watangazaji Irene Gabriel na Agape Msumari  ndani ya studio za City FM 

No comments