AUDIO: MELODY MBASSA ATAJA MALENGO YA LADHA YA UPANDE WA PILI YA “NIKUKOLEZE”


Melody Mbassa, mwimbaji anayeinukia vizuri kwenye muziki kiafrika hususan rumba, amesema hatua yake ya kutoa toleo la miondoko ya ‘zouk’ ya nyimbo yake “Nikukoleze”, ni ya kibiashara zaidi.

Mbassa akiongea katika ofisi za Saluti5, akasema hiyo ni sehemu ya mpango wa kuhakikisha kuwa ngoma yake hiyo inawashika watu wa kila aina.

“Toleo la kwanza lilikuwa katika miondoko ya rumba, ila hii za zouk ni kwaajili ya kupenya hadi kwenye soko la bongo fleva,” alisema Melody Mbassa.

Isikilize “Nikukoleze” iliyopigwa katika miongoko ya zouk.

No comments