AUDIO: SAKATA LA RAHMA MACHUPA …WASIKILIZE THABIT ABDUL, RAHMA NA AMIGO WALIVYOFUNGUKA RADIONI …sheria kuchukua mkondo wake, kazi ipo!


Baada ya Jumamosi usiku Jahazi kumtangaza Rahma Machupa kama msanii wao mpya huku Saluti5 ikiwa ya kwanza kuripoti tukio hilo, sakata hilo limezidi kuchukua sura mpya.

Sasa sheria inatarajiwa kuchukua mkondo wake na muda mfupi ujao mbivu na mbichi zitajulikana.

Inasemekana Rahma Machupa ana mkataba wa miaka miwili Wakali Wao na bado haujaisha, lakini yeye mwenyewe anasema mkataba wake umemalizika, Jahazi nao wanasema wao hawahusiki na mambo ya mkataba.

Capital Radio ya jijini Dar es Salaam kupitia kipindi chake cha Jiachie kinachoruka kila Jumapili saa 12 jioni hadi 3 usiku, kiliwahoji Thabit Abdul, Rahma Machupa na Prince Amigo ambapo kila mmoja alifunguka vizuri sana. Hebu wasikilize kupitia audio tuliyokuwekea hapo chini.

No comments