AUDIO: VICTOR NKAMBI ASIMAMISHWA TWANGA PEPETA MIEZI MIWILI … ‘tutamuona’ mwaka ujao panapo majaaliwa


Mpapasa kinanda wa Twanga Pepeta Victor Nkambi amesimamishwa kuitumikia bendi hiyo kwa miezi miwili.

Hiyo maana yake ni kwamba msanii huyo kuonekana kwenye jukwaa la Twanga Pepeta ni hadi mwaka ujao Mungu akipenda.

Kisa? Asha Baraka, mkurugenzi wa Twanga, ameiambia Saluti5 kuwa sababu kubwa ni ukosefu wa nidhamu na kuongoza harakati za kuididimiza bendi huku yeye akiwa ni mmoja wa viongozi wa Twanga Pepeta.

Halafu pia kumbe Victor hachangagi kabisa pale wenzake wanapokuwa na matatizo kama ya misiba au kuuguliwa, yaani jamaa ni ‘nati’ ile mbaya.

Hebu msikilize Asha Baraka anavyofafanua makosa ya Victor Nkambi na adhabu aliyompa.

No comments