AUGUST ALSINA AJISAFISHA KWA MASHABIKI LAWAMA ZA KUCHELEWESHA ALBAMU MPYA

BAADA ya mashabiki wa mkali wa R&B, August Alsina, kulalamika juu ya albamu yake kuchelewa kutoka, mkali huyo ameishukia lebo ya Def Jam kuwa ndiyo inayochelewesha kutoa mzigo huo.

Alsina alijibu malalamiko hayo ya mashabiki zake kwenye mtandao wa Twitter, akiitaja moja kwa moja lebo hiyo na kusema mwakani ndio itatoka rasmi lakini kama kila kitu angekisimamia yeye angehakikisha inatoka mapema.

“Def Jam ndio wanaochelewesha kazi. Sababu kuu ni kwamba mwakani ndio watarudi ofisini lakini kiukweli sijapendezwa nao. Nitatoa miziki kadhaa ya bure lakini najaribu kuwaomba Def Jam waiachie albamu yangu tu,” aliandika.


Mzaliwa huyo wa New Orleans ameachia ngoma nne za maandalizi ya albamu hiyo ambazo ni ‘Wait’, ‘Lonely’, ‘Don’t Matter’ na ‘Drugs’.

No comments