BAADA YA KUVUNJIKA PUA, SERGIO RAMOS ASEMA: 'KWA TIMU HII NITAVUJA DAMU MARA 1000'Sergio Ramos amedai atarejea dimbani muda si mrefu baada ya kuvunjika pua kwenye mechi ya 'watani wa jadi' dhidi Atletico Madrid Jumamosi usiku, mchezo ulioisha kwa sare ya 0-0.

Kikosi cha Zinedine Zidane kililazimika kucheza kwa kipindi chote cha pili bila nahodha wao huyo baada ya kuumia na kutolewa nje kufuatia kugongana kwake na Lucas Hernandez wa Atletico.

Ramos akatupia picha zake zilizotapakaa damu Instagram na kuandika: "Nitavuja damu mara 1000 kwaajili ya timu hii. Asanteni kwa sapoti yenu. Nitarejea dimbani muda si mrefu #HalaMadrid".


No comments