BAADA YA NEMANJA MATIC, MAN UNITED SASA YAMVIZIA DAVID LUIZ


Jose Mourinho bado haamini ukubwa wa safu yake ya ulinzi ya Manchester United na sasa inaaminika kuwa mpango wake wa kumwania beki wa Chelsea David Luiz, si jambo la maskhara.

Mourinho anatafuta upenyo wa kumshawishi beki wa Chelsea, David Luiz ambaye hana maelewano mazuri na klabu yake ili kumsajili dirisha la Januari.

David Luiz, raia wa Brazil ameanza kusugua benchi Chelsea baada ya kuzinguana na kocha wake Antonio Conte ambaye hapepesagi macho  pale anapoamua kumsulubu mchezaji wake.

Mourinho anataka kutumia mgogoro wa Conte na Luiz mwenye umri wa miaka 30 kama chambo cha kukamilisha dili hilo.

No comments