BARCELONA WATIA DOA REKODI YAO YA MIAKA MITANO LIGI YA MABINGWA


Haijawahi kutokea ndani ya miaka mitano iliyopita kwa Barcelona kutoka uwanjani bila bao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi.

Lakini Jumanne usiku Olympiakos ya Ugiriki ikavunja mwiko huo kwa kulazimisha sare ya 0-0 katika mchezo wa kundi D dhidi ya miamba hiyo ya Hispania.

Hata hivyo, Barca bado inaongoza kundi D kwa tofauti pointi tatu baada ya Juventus kupata sare ya 1-1 na Sporting Lisbon.

No comments