BARCELONA YAMTAKA GREIZMANN KUZIBA PENGO LA NEYMAR

KLABu ya Barcelona iko tayari kumsajili mchezaji wa Atletico Madrid, staa Antoine Griezmann katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari.

Barcelona wameandaa dau la pauni mil 89 ili kukamilisha usajili wa staa huyo raia wa Ufaransa ambaye pia alikuwa akiwindwa na Jose Mourinho.


Tangu kuondoka kwa Neymar Barcelona imekuwa ikihaha kusaka staa mwenye hadhi ya dunia atakayeziba nafasi yake vizuri.

No comments