BAYERN MUNICH YAIFUMUA BORUSSIA DORTMUND 3 -1


Bayern Munich imezidi kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga) baada ya kuwafunga wapinzani wao wakubwa Borussia Dortmund 3-1.

Ikicheza ugenini, Bayern ikawafunika wapinzani wao kila idara na iliwachukua dakika 17 tu kabla ya kuandika bao la kwanza kupitia kwa Arjen Robben.

Robert Lewandowski akatupia bao la pili dakika ya 37 huku David Alaba akiandika goli la tatu dakika ya 67 kabla wenyeji hawajapata bao la kufutia machozi dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika kupitia kwa Marc Bartra.

No comments