BAYERN MUNICH YANAWA MIKONO KWA ALEXIS SANCHEZ

KLABU ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani imeripotiwa kufuta mpango wa kumnasa mshambuliaji wa timu ya Arsenal, Alexis Sanchez mwenye miaka 28.

Klabu hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuwa Sanchez ameshafanya mkakati wa kuhamia kwenye timu nyingine tofauti na yao.

Staa huyo wa Chile anahusishwa kutaka kujiunga na timu ya Manchester City baada ya mkataba wake kumalizika mwishoni mwa msimu huu. 

No comments