BENCHI LAMCHOSHA DANIEL STURRIDGE LIVERPOOL... apanga kuondoka "mchana mchana"

MSHAMBULIAJI wa timu ya Liverpool, Daniel Sturridge ameweka wazi mpango wake wa kutaka kuondoka katika kikosi hicho baada ya kukosa namba ya kudumu.

Msimu uliopita alikuwa nyota muhimu lakini tangu apate majeraha amekuwa hana nafasi tena katika kikosi cha kwanza.


Sturridge mwenye miaka 28, amedai kuwa anatafuta timu itakayompa muda wa kucheza ili aweze kurejesha kiwango chake cha zamani.

No comments