BENCHI LAMCHOSHA DAVID LUIZ SASA ANUKIA REAL MADRID USAJILI WA DIRISHA DOGO LA JANUARIBeki wa Chelsea David Luiz, anatajwa kuwa yuko mazungumzoni na Real Madrid juu ya uwezekano wa kujiunga na miamba hiyo ya Hispania katika dirisha la usajili la mwezi Januari.

Nyota huyo wa kimataifa wa Brazil amekuwa si chaguo la kwanza la Antonio Conte baada ya ‘kubwatukiana’ na kocha huyo wa Chelsea katika kichapo cha 3-0 dhidi ya Roma mwishoni wa mwezi Oktoba kwenye mchezo wa Champions League.

Inaaminika David Luiz mwenye umri wa miaka 30, alikosoa mbinu za ufundishaji za Conte kwenye mazoezi ya maandilizi ya mchezo uliofuata dhidi ya Manchester United.

Kuanzia hapo David Luiz akasugua benchi katika mechi za Premier League dhidi ya Manchester United, West Brom na Liverpool.

Kwa mujibu wa RMC Sport Luiz anahusishwa na mazungumzo ya kujiunga na Real Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane.

No comments